Pata taarifa kuu
KENYA

Majeshi ya Kenya yaua zaidi ya wapiganaji 60 wa Al Shabab

Majeshi ya Kenya yamefanikiwa kuwaua zaidi ya wapiganaji 60 wa kundi la Al Shabab kusini mwa Somalia katika mapambano ya anga.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Kenya kanali Cyrus Oguna amesema mashambulizi hayo yalifanikiwa kupiga eneo la waasi hao huko kusini mwa Somalia eneo la Gedo.

Wakati huohuo Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Uingereza imeonya wageni nchini Kenya, juu ya kuwepo kwa tishio kubwa la mashambulio ya kigaidi.

Wizara hiyo imesema inaamini kuwa magaidi wanaweza kuwa katika hatua za mwisho za mpango wa kufanya mashambulio, na kwamba wageni waepuke maeneo ambayo yenye mikusanyiko ya watu kama vile nyumba za starehe,madukani na ufukweni.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.