Pata taarifa kuu
Ethiopia

Umoja wa Mataifa waombwa kuongeza Askari zaidi kuboresha Operesheni dhidi ya Al Shabaab

Umoja wa Afrika umeutaka Umoja wa Mataifa kuidhinisha ongezeko la vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, ambapo kiasi cha askari 17,700 wanahitajika baada ya kuwepo kwa mashambulio yanayofanywa na waasi wa kiislam.

Rais wa Somalia, Sharif Sheikh Ahmed
Rais wa Somalia, Sharif Sheikh Ahmed REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Kenya ndani ya Umoja wa Mataifa, Monica Juma amesema kuwa majeshi ya AMISOM yamekuwa yakifanya kazi chini ya Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2007 na kwamba hivi sasa wanahitaji vikosi vingine kwa ajili ya kuangalia hali ya usalama wa maeneo yaliyowekwa huru dhidi ya waasi.
 

Hivi sasa Jeshi la AMISOM lina vikosi kutoka Djibouti, Uganda na Burundi walio nchini Somalia tangu mwaka 2007 ili kulinda serikali dhidi ua makundi ya waasi wa Al Shabaab.

Kamishna wa maswala ya Amani na usalama Ramtane Lamamra amesema kuwa vikosi vya Afrika wako tayari kabisa kupambana na Al Shabaab na maharamia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.