Pata taarifa kuu
Nigeria

Watu sita wauawa kwa risasi walipokuwa wakiabudu huko Kaskazini mwa Nigeria

Watu sita wameuawa katika shambulio la risasi lililotekelezwa na watu wenye silaha dhidi ya waumini wa kikristo waliokuwa wakiabudu katika kanisa moja nchini Nigeria.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan REUTERS/ Daniel Munoz
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea nje ya mji wa Gombe kaskazini mwa Nigeria baada ya muda ulioamriwa kwa wakristo kuondoka maeneo ya kaskazini na kurejea kusini.
 

Hata hivyo hakuna yeyote aliyeshkiwa kuhusika na shambulio hilo la usiku wa kuamkia leo dhidi ya kanisa la Deeper Life Christian Ministry Church.
 

Katika hatua nyingine, Polisi nchini Nigeria wamewazuia waandamanaji waliokuwa wamepanga kuandamana mjini Abuja hii leo wakipinga kupanda kwa bei ya mafuta, hatua iliyoleta ghadhabu kwa raia wa nchi hiyo.

Takriban waandamanaji 40 walikuwa wakitarajia kuandamana hadi katika viwanja vya Eagle mjini abuja kisha kuzuiwa na polisi wakiwa njiani kuelekea katika viwanja hivyo.
 

Hatua hiyo ya polisi ni inalenga kukomesha maandamano yanayoanza kushika kasi hasa baada ya hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya Mafuta terehe moja mwezi huu, na kusababisha mafuta kupanda bei mara mbili zaidi.
 

Leo hii mjini Kano polisi wanadaiwa kuwa walimwaga gesi ya machozi na kuwapiga waandamanaji,madai yanayopingwa na mamlaka ya nchini humo.
 

Shirika la kimataifa linaloshughulikia maswala ya haki za binaadam la Amnesty International limetaka mamlaka ya Nigeria kutotumia nguvu dhidi ya waandamanaji.
Raia wa Nigeria wamepanga kufanya mgomo wa kitaifa juma lijalo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.