Pata taarifa kuu
Misri

Zoezi la upigaji kura za wawakilishi wa Bunge zaendelea hii leo nchini Misri

Zoezi la upigaji kura limeendelea nchini Misri ambapo siku ya jumatano ndiyo hatma ya uchaguzi huo wa bunge la kwanza tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa kiongozi wa misri Hosni Mubarak mnamo mwezi Februari.

Reuters/Asmaa Waguih
Matangazo ya kibiashara

Katika siku ya pili ya kupiga kura Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema asubuhi katika majimbo mbalimbali nchini humo huku wananchi wakiwa katika mistari michache ya kuelekea kupiga kura.
 

Vyama vya kiislamu vilivuna ushindi wa kimgogoro katika awamu mbili za kwanza za uchaguzi ambao ulianzia katika maeneo mengine ya nchi mnamo novemba 28 mwaka jana tangu ukanda wa kiarabu uingie katika mapambano ya kupindua utawala wa kimabavu.
 

Baraza tawala la kijeshi lililochukua madaraka baada ya kupinduliwa kwa Hosni Mubarak mwezi Februari litateua wabunge 10 huku chama cha kiislamu chenye uzoefu wa kupanga harakati za kisiasa nchini humo Freedom and Justice party,FJP kimedai kitaongoza kwa kupitia mkono wake wa siasa.
 

Baraza Kuu la Vikosi vya majeshi (SCAF)limesema kuwa uchaguzi umekuwa kama uthibitisho wa nia yake ya kuukabidhi uongozi kwa serikali ya kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.