Pata taarifa kuu
Angola

Rais wa Angola atangaza kuhakikisha uchaguzi wa mwisho wa mwaka ujao unakuwa huru na haki

Rais wa Angola Jose Eduardo Dos Santos amejiapiza kuhakikisha nchi yake inajiandaa na hatimaye kufanya uchaguzi huru na wa haki utakaofanyika mwishoni mwa mwaka elfu mbili na kumi na mbili.

Rais wa Angola Dos Santos
Rais wa Angola Dos Santos
Matangazo ya kibiashara

Rais Dos Santos amesema kwa sasa mchakato wa uchaguzi huo mkuu watatu umeshaanza kwani baadhi ya vyama vimeshatangaza wagombea wake huku vingine vikiwa vimetangaza nia ya kusimamisha wagombea.

Upinzani mkubwa unatarajiwa kushuhudia kati ya Chama Tawala cha Rais Dos Santos cha MPL na kile cha UNITA kilichokuwa kinaongozwa na Marehemu Jonas Malheiro Savimbi ambaye alikuwa anaongoza mapambano dhidi ya serikali wakati wa uhai wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.