Pata taarifa kuu
MISRI

Duru la Pili la Uchaguzi la Wabunge lafanyika nchini Misri tangu kuangushwa kwa Rais Mubarak

Wananchi wa Misri wanatumia haki yao ya Kikatiba kuchagua Wabunge wao ikiwa ni duru la pili la Uchaguzi nchini humo kufanyika kidemokrasia tangu kuangushwa kwa Utawalawa wa Rais Hosni Mubarak.

Reuters/Asmaa Waguih
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya wananchi wamejitokeza kutumia haki hiyo ya msingiukiwa ni muendelezo wa mchakato wa kufika kikomo kwa Utawala wa Kijeshi chini ya Field Marshal Mohammed Hussein Tantawi.

Chama Cha Muslim Brotherhood ambacho kilipata ushindi wa asilimi thelathini na mbili katika uchaguzi wa wabunge kinapewa nafasi kubwa ya kuendeleza wimbi lake la ushindi kwenye uchaguzi huu wa leo.

Duru la pili ni matokeo ya kushindwa kupatikana mshindi wa jumla kwenye kinyang'anyiro cha awali ambapo sasa wapigakura wapatao milioni kumi na nane nukta nane watashiriki kwenye uchaguzi huo muhimu.

Wapigakura nchini Misri watakuwa na kibarua cha kupiga katika masanduku matatu tofauti ambao moja litakuwa la wagombea binafsi, jingine la wagombea wa vyama na lile la mwisho ni la vyama ambavyo vimeungana.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mapema saa mbili asubuhi huku baadhi ya wapigakura waliotekeleza haki hiyo ya kikatiba wakisema wamefurahishwa kwa kupata fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Nchi ya Misri imefanya uchaguzi wake wa kidemokrasia baada ya nguvu ya umma kutumika kuuangushwa Utawala wa zaidi ya miongo mitatu wa Rais Hosni Mubarak ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya kujibu ikiwemo ubadhirifu na kuamrisha mauaji ya waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.