Pata taarifa kuu
DRC

Vituo vya kupiga kura vyafunguliwa tena hii leo huku kura zikihesabiwa, DRC

Wakati zoezi la kuhesabu kura likiwa limeanza hii leo, Vituo vya kupiga kura vimefunguliwa tena hii leo nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC huku maelfu ya wapiga kura wakitarajiwa kupiga kura baada ya hapo jana kushindwa kufanya hivyo.

Zoezi la kupiga kura likiendelea nchini DRC
Zoezi la kupiga kura likiendelea nchini DRC Reuters/Finbarr O'Reilly
Matangazo ya kibiashara

Tume huru ya uchaguzi ya taifa hilo, CENI imetangaza jana kuwa kura zitapigwa tena hii leo maalum kwa ajili ya walioshindwa kupigwa kura siku ya jana baada ya kuwepo kwa misururu mirefu iliyokuwa ikiongezeka mpaka wakati wa kufunga vituo.
 

Takriban raia milioni 32 wa Congo waliwasili katika vituo mbalimbali vya kupiga kura nchi nzima huku kukiwa na taarifa za kuwepo kwa vurugu kati ya wafuasi wa upinzani mjini kinshasa na shambulio katika vituo vya kupiga kura mjini Lubumbashi.
 

Ingawa zoezi la kupiga kura lilichelewa kuanza, wapiga kura walivumilia ili kuweza kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.