Pata taarifa kuu
Afrika Kusini

Julius Malema kukata rufaa ANC

Aliyekuwa kiongozi wa vijana ndani chama kinachoongoza nchini Afrika kusini African National Congress, ANC Julius Malema ameapa kukata rufaa dhidi ya adhabu aliyopewa ya kusimamishwa kwenye chama hicho na kamati ya nidhamu ya Chama hicho.

REUTERS/Siphiwe Sibeko/Files
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na vyombo vya habari ikiwa ni takriban wiki moja baada ya matokeo ya kesi yake, na kudai kuwa hakutendewa haki.

Kamati ya nidhamu ya ANC ilimpa adhabu Malema ya kutoshiriki shughuli zozote za kisiasa ndani ya ANC kwa muda wa miaka mitano,kwa kukashifu utawala wa rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma halikadhalika madai ya kukigawa chama.

Kamati nyingine ya ANC itasikiliza madai ya Malema ambayo ameeleza kuwa adhabu hiyo imelenga kummaliza kisiasa.

Kusimamishwa urais wa vijana na amri ya kuondoka madarakani hakutatekelezwa isipokuwa baada ya kuidhinishwa na kamati ya rufaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.