Pata taarifa kuu
Tunisia-Uchaguzi

Wananchi wa Tunisia wapiga kura Jumapili hii

Wananchi nchini Tunisia wamepiga kura jumapili hii kuwachagua wabunge 217 wataowakilisha bunge nchini humo. Huu ni uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia na ki historia kufanyika nchini humo tangu kuangushwa kwa utawala wa rais Ben Ali mwezi Januari iliopita. Jumla wagombea elfu kumi na moja ndio wanawania nafasi hizo.

Wananchi wa Tunisia wakidiriki shughuli za upigaji kura, 23/10/2011
Wananchi wa Tunisia wakidiriki shughuli za upigaji kura, 23/10/2011 REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Chama tawala zamani nchini humo kilifutwa na kutowa nafasi kwa vyama vipya ambavyo vimewasilisha wagombea si chini ya elfu kumi na moja, kuwania nafasi ya wabunge 217

Bunge hilo baada ya kuchaguliwa litakuwa na jukumu la kulinda sera za wanaharakati, na kujadili kuhjuus mfumo wa uteuzi wa rais. Hadi hapo rais wa sasa na serikali yake wataendelea kutawala hadi pale bunge jipya litapo afiki kuhusu uteuzi wa rais na mfumo mzima wa uongozi katika taifa hilo ambalo ndilo kitofu cha wanaharakati katika nchi za kiarabu.

Mbali na majukumu hayo ya bunge, wabunge hao watatakiwa pia kuunda katiba mpya ya nchi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.