Pata taarifa kuu
Nairobi kenya

Muili wa profesa Wangari Mathai wateketezwa kama ilivyo tarajiwa

Mwili wa Profesa Wangari Maathai umechomwa kama alivyopendekeza yeye mwenyewe wakati wa uhai wake. Kamati iliyochaguliwa ili kupanga mazishi ya Wangari Maathai imesema kuwa mwili wa mwanamazingira huyo utachomwa katika maziara ya Kariokor, siku ya Jumamosi wiki hii.

Wangari Maathai mwaka 2010
Wangari Maathai mwaka 2010 REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa kuendeleza kazi aliyoanzisha marehemu profesa wangari mathai ulitawala hii leo huku viongozi na wakenya wakitoa heshima zao za mwisho kabla ya kuteketezwa kwa mwili wake.

Wengi walisifia kazi ya kuboresha mazingira kupigania demokrasia na usawa wa jinsia ambazo marehemu alihusika nazo pakubwa. Maelfu ya watu walifurika katika bustani hiyo, wakiongozwa na viongozi mashuhuri waliohudhuria ni pamoja na rasi Mwaki Kibaki, waziri mkuu Raila Odinga na makamu wa rais Kalonzo Musyoka.

Ibada ya wafu ilifanywa kwenye bustani ya Uhuru Park, Nairobi, ambayo Wangari aliitetea sana wakati serikali ya Rais Moi ilipotaka kuruhusu majumba kujengwa katika bustani hiyo.

Na kwa wakati mmoja kulitokea sintofahamu huku wakenya waliofika katika makaburi ya keriako hapa mjini Nairobi wakishinikiza kuona mwili wa maathai kabla haujachomwa kinyume na mipango ya familia.

Wanaharakati wa mazingira na wanawake ambao walishirikiana na Bibi Maathai tangu alipoanza kampeni zake miaka ya 1970 piya walihudhuria, pamoja na wawakilishi kutoka nchi za nje.

Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Makaazi, Bibi Anna Tibaijuka, ambaye piya alikuwa rafiki wa Bibi Maathai; Sudan ilituma mwakilishi, na wanabalozi wa nchi kadha walihudhu

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.