Pata taarifa kuu
Misri-Marekani

Marekani yautaka utawala wa kijeshi nchini Misri kumaliza hali ya hatari nchini humo

Marekani inataka Misri kumaliza, hali ya hatari nchini humo haraka iwezekanavyo, na waziri wa nchi za kigeni wa Marekani Hillary Clinton amesema uongozi wa kijeshi nchini humo umeahidi kuondoa hali hiyo, kabla ya mwezi Juni mwaka ujao.

Jengo la Bunge la Misri jijini Cairo
Jengo la Bunge la Misri jijini Cairo AFP PHOTO/MAHMUD HAMS
Matangazo ya kibiashara

Bibi Clinton amesema kuwa, hali hiyo itasaidia kuimarisha hali ya demokrasia nchini humo, ikilinganishwa na wakati wa rais wa zamani Hosni Mubarak aliyeongoza taifa hilo kwa zaidi ya miaka thelathini.

Wakati hayo yakijiri, muungano wa kundi la kiislamu la Muslim Brotherhood wametishia kujiodoa katika uchaguzi wa wabunge mwezi Novemba mwaka huu, ikiwa kifungu cha sheria kuhusu uchaguzi hakitabadilishwa.

Kifungo hicho hakikubali vyama vya kisiasa kuchagua thuluthi tatu ya wabunge wakati wa uchaguzi wa wabunge nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.