Pata taarifa kuu
Burundi

Serikali ya Burundi yatangaza musba wa siku 3

Serikali ya burundi imetangaza musba wa siku 3 baada ya kutokea mashambulizi kwenye kilabu mojawapo cha pombe tarafani Gatumba umbaliw akilometa 15 na mji mkuu Bujumbura, karibu na mpaka wa Burundi na Jamuhiri ya kidemokrasia ya Congo maeneo ya Uvira. Watu 49 wamepoteza maisha katika shambuli hilo baya kuwa kutokea tangu ulipomalizika uchaguzi wa mwaka jana.

Isanganiro
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo la kundi la watu wanaosadikiwa kuvalia sare za polisi na silaha nzitonzito, lilitokea usiku wa Jumapili saa mbili na kudumu muda wa dadakika 20.

Kulingana na mashahidi watu kadhaa walikuwa katika klabu mojawapo ya pombe tarafani hapo Gatumba ijulikanayo kama kwa β€œchez les amis” muda mfupi wakaona kundi la watu waliovalia sare za polisi waliowalazimisha kulaza matumbo yao chini, na kuanza kuvurumisha guruneti na risase. Baada ya operesheni hiyo, watu hao waliondoka bila wasiwasi yoyote kwani, wanajeshi wa serikali ywaliwasili eneo hilo watu hao wamekwisha ondoka.

Watu zaidi ya 30 walifariki papo hapo wengine walifia hospitalini wakati ma dactari walipojaribu kuokoa maisha yao.

Viongozi mbalimbali wamejitokeza katika eneo la tukio kushuhudia. Mpatanishi katika mizozo baina ya serikali na wananchi Onmbusman Cheikh Muhamed Rukara, mawaziri wa serikali ya Burundi akiwemo waziri wa Ulinzi na wa Usalama wa raia, ma balozi wa Ubelgiji, Ufaransa, Ujerumani pamoja na katibu mkuu wa secretariate ya maziwa makuu.

Viongozi wa mashirika ya kiraia pia walikuwepo kwenye eneo la tukio ambao wamelaani vikali tukio hilo ambao wameomba uchunguzi uanzishwe mara moja kujuwa wahusika wa tukio hilo.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ambae alizuru kwenye eneo la tukio, ametangaza musba wa siku tatu, na kuahirishwa kwa msafara wake nchini Marekani. Rais huyo ametowa muda wa siku 30 kwa vyombo vya sheria kuwa vimekamilisha uchunguzi, kabla ya kutangaza kwamba gharama ya shughuli za mazishi na matibabu kwa majeruhi, itakuwa chini ya serikali ya Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.