Pata taarifa kuu
Nigeria

Mtu mwenye silaha, awashambulia watu na kuwauwa katika mji wa Borno kaskazini mwa Nigeria

Watu wanne wamekufa papohapo na wengine kadhaa wamejeruhiwa nchini Nigeria kufuatia mtu mmoja mwenye silaha kuwafyatulia risasi watu hao kwenye mji wa Borno kaskazini mwa nchi hiyo.

trendsupdates
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Polisi katika eneo hilo Simeon Midenda amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mtu aliyefanya tukio hilo bado hajakamatwa na anahisiwa kuwa ni kutoka kundi la kiislamu la Boko Haram.

Nchi ya Nigeria imeendelea kuwa katika hali ya sintofahamu kufuatia machafuko yanayoendelea katika miji mbalimbali nchini humo ukiwemo mji wa Jos ambako kuna mapigano ya mara kwa mara kati ya waislamu na wakristo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.