Pata taarifa kuu
Afrika kusini

Julius Malema akutwa na hatia

Mahakama ya Afrika kusini imethibitisha kuwa kiongozi wa vijana chini ya mwamvuli wa chama cha African National Congress ANC, Julius Malema ana hatia kwa makosa ya kutoa maneno yanayoelezwa kuwa na uchochezi katika wimbo wa kupiga vita ubaguzi wa rangi nchini humo.

Julius Malema, kiongozi wa vijana wa chama tawala nchini Afrika kusini l’ANC
Julius Malema, kiongozi wa vijana wa chama tawala nchini Afrika kusini l’ANC RFI
Matangazo ya kibiashara

Jaji wa mahakama hiyo amesema kuwa kuimbwa kwa wimbo huo kunachochea chuki baina ya raia wa nchi hiyo na kumpiga marufuku Malema na chama chake kuuimba wimbo huo.

Wakati kesi ya Malema ikitolewa uamuzi,mahakama nyingine imesema kuwa wimbo huo ulikuwa unachochea mauaji na chuki kati ya watu weupe na weusi.

Kesi iliyoamuliwa na mahakama hiyo ni tofauti na ile inayosikilizwa na kamati ya nidhamu ya ANC,kwa shutma za kukigawa chama.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.