Pata taarifa kuu
Tanzania-Zanzibar

Watu 610 wazama, 250 waokolewa wakiwa hai kisiwani Zanzibar

Watu 610 waliokuwa katika meli ya Mv Spice Islanders wanahofia kufa baada ya meli hiyo kuzama mkondo wa Nungwi ikielekea Pemba katika bahari ya hindi usiku wa jana kuamkia leo Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Meli hiyo ya Mv Spice Islanders iliondoka katika badari ya Malindi kisiwani Unguja ikiwa katika hali nzuri, lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubinuka na hatimae kuzama.

Duru za serikali zaarifu kuwa ajali hiyo ilitokea mida ya saa nane na nusu za usiku wa kuamkia leo na abiria 610.

Hadi sasa imearifiwa kuokolewa kwa watu 250 wakiwa hai. Serikali na watu binafsi wanaendelea na juhudi za kuwatafuta watu walikuowemo katika ajali hiyo aidha wangali hai au wamekufa.

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Ali Mohamed Shein amejielekeza katika eneo la tukio huku Nungwi kushuhudia shughuli za uokozi zinazoendelea

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.