Pata taarifa kuu
Misri

Mawakili watwangana mahakamani wakati kesi ya Mubarak ikisikilizwa

Mashambulizi yamezuka nje ya mahakama ya Cairo, Misri wakati kesi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak ikiendelea kusikilizwa leo huku watu wakirushiana mawe na kusababisha majeruhi.

Reuters/Egypt TV
Matangazo ya kibiashara

 

Ndani ya mahakama kesi hiyo ililazimika kusimama baada ya dakika 40 tangu kuanza kusikilizwa na mawakili wa pande za utetezi na mashitaka wakilazimika kutenganishwa na polisi kutokana na kuzuka kwa vurugu.
Kufuatia vurugu hizo ndani na nje ya mahakama watu wasiopungua 12 wamekamatwa wakiowemo wanaompinga Mubarak na wale wanaomuunga mkono kiongozi huyo wa zamani wa Misri.
Vurugu katika mahakama hiyo zilianza baada ya watu waliokuwa katika eneo hilo kuanza kurusha mawe kwa polisi na watu wakionyesha hisia zao kutokana na kufikishwa tena mahakamani kwa Mubarak.
Ndani ya mahakama hiyo jaji anayeendesha kesi hiyo alilazimika kusitisha kwa muda kesi hiyo baada ya mawakili wa pande hizo mbili kuanza kurushiana ngumi.
Mubarak aliwasili katika eneo la mahakama kwa helkopta na kesi hiyo ikisikilizwa kwa siri na watu kushindwa kushuhudia kama ilivyokuwa wakati wa kusikilizwa kwa shauri kwa mara ya kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.