Pata taarifa kuu
Somalia

Viongozi wa Afrika wakutana kusaidia Somalia, Pembe ya Afrika

Viongozi wa nchi za Afrika wanakutana hii leo mjini Adis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kusaidia zaidi ya watu milioni kumi na mbili katika Pembe ya Afrika waliokumbwa na ukame na baa la njaa.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa mataifa umetangaza kukithiri kwa hali ya njaa kwa miaka mitano nchini Somalia huku mamilioni ya watu wakitafuta hifadhi nchini Ethiopia,Djibouti,Kenya na Uganda,kutokana na ukame.
Nchi ya Somalia ni nchi ambayo imeathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na hali hiyo na hali ya mapigano na machafuko baina ya Serikali na kikundi cha Al-Shabab yameongeza uzito wa tatizo hilo la njaa kwa kuwa badhi ya maeneo hayafikiki kirahisi.
Mkuu wa tume ya umoja wa Afrika Jean Ping, amewataka waafrika kulitafutia ufumbuzi tatizo la njaa kwa kuchangia kwa fedha zitakazo saidia kuokoa maisha ya waafrika katika pembe ya Afrika.
Kiasi cha euro bilioni 1.6 kinahitajika kusaidia waathirika wa baa la njaa na ukame takriban milioni kumi na mbili nukta nne,huku umoja wa Afrika umeahidi kuchangia kiasi cha dola za kimarekani laki tano.
Mpaka hivi sasa serikali chache za kiafrika zimeahidi kuchangia dola milioni 21,huku waratibu wa mchakato wa uchangishaji fedha wakisema nchi za Kiafrika zinapaswa kuchangia kiasi kisicho chini ya dola milioni 50.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.