Pata taarifa kuu
Cape Verde-Uchaguzi

Mgombea wa upinzani ashinda duru ya pili ya uchagugu Cape verde

Mgombea nafasi ya urais kutoka upinzani, Jorge Carlos Fonseca ameshinda duru ya pili uchaguzi wa urais nchini Cape Verde ikiwa ni taarifa kwa mujibu wa kura zinazoelekea ukingoni kumalizika hesabu yake,kura zilizotangazwa leo na vyombo vya habari.

Jorge Carlos Fonseca  Praia,  20 Agosti 2011.
Jorge Carlos Fonseca Praia, 20 Agosti 2011. . AFP / SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Fonseca aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ameshinda kwa asilimia 54.53 ya kura zilizopigwa hapo jana dhidi ya hasimu wake Manuel Inocencio Sousa,aliyepata asilimia 45.47 ya kura,kwa mujibu wa matokeo kutoka asilimia 92 ya vituo vya kupiga kura.

Fonseca kutoka chama cha upinzani cha Movement For Democracy (MFD),alishinda kwa zaidi ya asilimia 37 ya kura zilizopigwa katika duru la kwanza la uchaguzi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.