Pata taarifa kuu
LIBYA

Vikosi vya Kanali Gaddafi vyaelezwa kutumia makombora ya masafa marefu mjini Brega

Wanajeshi watiifu kwa serikali ya kanali Muammar Gaddafi wamefanya mashambulizi kwa kutumua makombora ya masafa marefu “skadi” ikiwa ni mara ya kwanza kwa vikosi hivyo kutumia silaha za aina hiyo kuwasahmbulia waasi wanaopigana na serikali yake.

Waasi wa Libya wakiwa katika operesheni mjini Brega
Waasi wa Libya wakiwa katika operesheni mjini Brega Reuters/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Taarifa za vikosi vya serikali ya Libya kutumia silaha hizo imetolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Marekani ambayo imedai kuwa ni nadra sana kwa silaha hizo kutumika ikiwa zilipigwa marufuku kutumika katika vita.

Makombora hayo yalirushwa na vikosi vya serikali tokea katika mji wa Sirte uliojirani na mji wa Brega ambao waasi wanaopigana na serikali wamedai kushikilia baadhi ya maeneo ya mji huo.

Mpaka sasa serikali ya Libya haijasema chochote kuhusiana na taarifa hizo ingawa waasi wamekiri kuona makombora hayo ya masafa ,arefu katika maeneo ambayo yameshambuliwa na kudai kuwa hakuna mtu aliyeuawa wala kujeruhiwa.

Mashambulizi ya wanajeshi wa Kanali Muammar Gaddafi yamekuja kufuatia waasi wa nchi hiyo kuendelea kusonga mbele kuelekea mji mkuu Tripoli ambapo sasa wameanza mashambulizi katika mji wa Zawiya ulioko km 50 toka mji mkuu Tripoli.

Siku ya Jumatatu kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi aliwahutubia wananchi wake kupitia vipaza sauti ambapo waliwataka kujiandaa kwaajili ya vita, vita alivyoviita ni dhidi ya magaidi abao ni waasi na majeshi ya NATO yanayotaka kuchukua mali halali za mababu zao.

Wakati huohuo mazungumzo yanayosimamiwa na ujumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, mazungumzo yanayifanyika nchini Tunisia yameendelea ambapo ujumbe huo unakutana na viongozi wa serikali na wale wa waasi kujaribu kutafuta suluhu ya mgogoro wa Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.