Pata taarifa kuu
Somalia

Kamanda wa vikosi vya AU atoa wito wakupeleka vikosi zaidi nchini Somalia

Mkuu wa vikosi vya majeshi ya Umoja wa Afrika nchini nchini Somalia meja jenerali Fred Mugisha ametoa wito wa kuongezwa kwa vikosi zaidi nchini humo kufuatia wanamgambo wa Al shabab kuondoka mjini Mogadishu.

Markacaday
Matangazo ya kibiashara

Meja Mugisha amesema kuwa bado hali ya usalama mjini Mogadishu sio ya kuridhisha licha ya wapiganaji hao kuondoka na kuongeza kuwa kunahitajia vikosi zaidi ili kulinda usalama wa raia pamoja na maghala ya chakula cha msaada.

Wakati huohuo serikali ya nchini humo imewataka wapiganaji wa Al Shabab waliobakia mjini Mogadishu kusalimisha silaha za na kuwa serikali haitawachukulia hatua wito ambao mpaka sasa haujatekelezwa na wapiganaji hao.

Mwishoni mwa juma msemaji wa Al Shabab alitangaza kuviondoa vikosi vyake mjini Mogadishu na kuahidi kureja kwa nguvu ndani ya siku zijazo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.