Pata taarifa kuu
SOMALIA-MOGADISHU

Watu 7 wadhibitishwa kufa mjini Mogadishu Somalia baada ya mashambulizi ya risasi katika kambi ya Badbaado

Watu zaidi ya saba wamedhibitishwa kufa nchini Somalia katika mji wa Mogadishu kufuatia kuzuka kwa mashambulizi toka kwa watu wasio fahamika katika kambi moja ya msaada ya Badbaado mjini Mogadishu.

Mmoja wa wananchi wa Somalia akiokota mabaki ya chakula cha msaada
Mmoja wa wananchi wa Somalia akiokota mabaki ya chakula cha msaada Reuters 路透社
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wananchi laki moja wa toka kusini mwa nchi hiyo wamekimbilia katika mji mkuu wan chi hiyo Mogadishu kupata msaada wa chakula kutokana na nchi hiyo kukumbwa na ukame.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa tukio hilo lilitokea wakati ambapo wafanyakazi wa mashirika ya kutoa msaada mjini Mogadishu wakiwa katika msafara wakipelea chakula katika kamb hiyo na ndipo kilipotokea kikundi cha watu wasiofahamika na kuanza kushambulia msafara huo na kuzua hofu.

Mpaka sasa mamlaka nchini Somalia hazijadhibitisha kama watu waliofanya shambulio hilo ni kutoka kundi la wanamgambo wa Al Shabab wanaoendeleza mapambano nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.