Pata taarifa kuu
Côte d’Ivoire

Rais wa Côte d’Ivoire azuru nchini Nigeria

Rais wa Côte d’Ivoire Alassane Ouattara ambaye ameitembelea nchini ya Nigeria amelishukuru taifa hilo kwa ushirikiano ambao waliutoa wakati wa ghasia zilizoibuka baada ya uchaguzi mkuu nchini humo.

Ado.ci
Matangazo ya kibiashara

Rais Ouattara anasema msimamo ambao ulioneshwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi ECOWAS Goodluck Jonathan kushinikiza Laurent Gbagbo aondokea madarakani ulikuwa ni msaada mkubwa sana.

Kiongozi huyo wa Côte d’Ivoire amesema hakika nchi yake ilipita kipindi kigumu sana ambacho kilichangia vifo vya watu zaidi ya elfu tatu pamoja na kuharibiwa kwa miundombinu muhimu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.