Kesi ya Hosni Mubarak kusikilizwa mjini Cairo
Kesi ya aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak itakayofanyika wiki ijayo huenda ikafanyika mjini Cairo, mbele ya familia za walioathiriwa na vitendo vya mauaji, vyombo vya habari nchini humo vimethibitisha.
Imechapishwa:
Vyanzo vya mahakama na ulinzi vilisema awali kuwa mubarak huenda atasomewa mashtaka yake yatasomwa sharm al sheikh anakoshikiliwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo yanayomkabili.
Waziri wa sheria wa nchi hiyo amethibitisha kesi ya mubarak na watoto wake kusikilizwa Cairo,na kuongeza kuwa ukumbi umetayarishwa kuwezesha mamia ya wanahabari, raia na familia za walioathiriwa na vitendo vya mauaji kuweza kupata nafasi ya kufuatilia kesi hiyo katika mahakama hiyo.