Pata taarifa kuu
SOMALIA-MOGADISHU

Wapiganaji wa Al Shabab nchini Somalia wamuachilia huru waziri waliyemteka

Hatimaye wapiganaji wa kundi la Al Shabab nchini Somalia, usiku wa kuamkia leo wamemwachia huru waziri wa Wanawake na Familia, Asha Osman Aqil baada ya kumteka siku ya jumatano katika eneo la Balad jirani na mji wa Mogadishu.

Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed akihutubia moja ya kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed akihutubia moja ya kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN Photo/Aliza Eliazarov
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kituo cha redio cha nchi hiyo, kimetangaza asubuhi ya hii leo kuwa wapiganaji hao wametangaza kumuachia huru kiongozi huyo baada ya kukubaliana na serikali.

Siku ya jumatano waziri mkuu wa Somalia Abdiwali Mohamed Ali alitangaza kutekwa kwa waziri huyo wakati akielekea kwenye moja ya mikutano yake ya awali ya baraza jipya la mawaziri lililotangazwa juma hili na rais Sheikh Sharif Ahmed.

Kufuatia tukio hilo ulinzi umeimarishwa maradufu mjini Mogadishu na kwenye makazi ya mawaziri wapya walioteuliwa kwa lengo la kuwazuia wapiganaji hao wa kiislamu kuteka viongozi zaidi.

Wakati huohuo mashirika ya misaada yaliyoko kusini mwa nchi hiyo kwenye maeneo yanayokaliwa na wapiganaji wa Al Shabab wamesema kuwa baada ya misaada kusimama kwa muda katika eneo hilo, wanatarajia kuanza tena kusamba za chakula kwa ndege kwenye maeneo ambayo wameshindwa kuyafikia.

Msemaji wa shirika la chakula duniani, Josette Sheeran ambaye yuko mjini Mogadishu kwa shughuli ya kugawa chakula, amesema kuwa walikuwa wanatarajia kufanya zoezi hilo kwa ufanisi lakini wamekwamishwa na wapiganaji wa Al Shabab wanaowateka hata wafanyakazi wa mashirika hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.