Pata taarifa kuu
Misri

Hakutokuwa na waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi wa bunge nchini Misri

Utawala wa kijeshi nchini Misri kwa mara ya kwanza umetangaza kuwa hautaruhusu waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi mkuu wa bunge unaotarajiwa kufanyika nchini humo mwaka huu.

Le maréchal Mohamed Hussein Tantaoui kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Misri
Le maréchal Mohamed Hussein Tantaoui kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Misri Reuters/Goran Tomasevic/Files
Matangazo ya kibiashara

Meja Jenerali Mamdouh Shaheen, ameweka wazi uamuzi wa baraza la kijeshi linaloongoza nchi hiyo siku ya jumatano wakati akitoa ripoti maalumu kuhusiana na sheria za uchaguzi zilizopitishwa na baraza hilo na kudai kuwa hakutakuwa na waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi wa wabunge.

Kiongozi huyo badala yake amesema kuwa uchaguzi mkuu utaangaliwa na kusimamiwa na waangalizi wa ndani hatua ambayo tayari wanaharakati nchini humo wamepinga na kutishia kuitisha maandamano makubwa.

Mbali na kupitishwa kwa sheria hiyo, pia baraza hilo limepunguza umri wa kuwania nafasi za ubunge toka miaka 30 hadi 25 ambapo pia rais atakayechaguliwa atateua wajumbe 100 wa bodi kati ya 390.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.