Pata taarifa kuu
Tunisia

Waziri mkuu wa Tunisia awataka wanaharakati kusitisha mipango ya maandamano

Kufuatia hofu ya kuzuka kwa machafuko mapya nchini Tunisia waziri mkuu wa nchi hiyo Beji Caid Essebsi amewataka raia wa nchi hiyo kusitisha maandamano ambayo wamepanga kuyafanya kushinikiza mabadiliko zaidi nchini humo.

Waziri mkuu wa Tunisia, Béji Caïd Essebsi.
Waziri mkuu wa Tunisia, Béji Caïd Essebsi. AFP/FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu Essebsi amesema kuwa kumekuwa na kila dalili ya baadhi ya watu wachache kuendelea kuchochea vurugu nchini humo kwa lengo la kutaka kuharibu mipango ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwezi wa kumi mwaka huu.

Kiongozi huyio ameyasema hayo wakati akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni siku ya jumatatu na kutoa wito kwa wananchi kuheshimu maamuzi waliyokubalina mara baada ya kuangushwa kwa utawala wa Ben Ali.

Wanaharakati na wananchi nchini Tunisia wamekuwa wakiituhumu serikali kwa kushindwa kuwachukulia hatua za haraka viongozi wa zamani waliokuwa chini ya utawala wa Ben Ali pamoja na kufanya mabadiliko ya mfumo wa kisiasa kama walivyoahidi awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.