Pata taarifa kuu
Afrika Kusini

Wafanyakazi nchini Afrika kusini wagoma kuomba nyongeza ya mshahara

Zaidi ya wafanyakazi elfu sabini wa viwanda vya mafuta nchini Afrika kusini hii leo wamejiunga katika mgomo wa wafanyakazi wa nchi nzima kushinikiza nyongeza ya mshahara.

Wafanyakazi wa nchini Afrika Kusini
Wafanyakazi wa nchini Afrika Kusini RFI
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la wafanyakazi wa viwanda vya mafuta nchini humo limesema kuwa wafanyakazi hao wanadai nyongeza ya mshahara wa kima cha chini cha randi elfu sita sawa na Euro 630 kwa mwezi ambao ni ongezeko la asilimia 13.

Kufuatia mgomo huo baadhi ya makampuni makubwa yanayosafisha mafuta nchini humo yamelazimika kufunga viwanda vyao kwa muda na kutishia kutokea kwa uhaba wa nishati hiyo nchini humo.

Tayari serikali ya nchi hiyo imetangaza kuingila kati mgogoro huo na kuahidi kufanyia kazi madai ya wafanyakazi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.