Pata taarifa kuu
BURKINA FASO - EU

EU yaitaka serikali ya Burkina Fso kufanya marekebisho ya sheria

Umoja wa Ulaya EU umeitaka serikali ya Bukinafaso kufanya marekebisho katika mfumo wake wa sheria na usalama kufuatia uasi wa mara kwa mara unaofanywa na wanajeshi dhidi ya Serikali.

Commision européenne à Bruxelles
Commision européenne à Bruxelles Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo ya umoja wa Ulaya inakuja ikiwa ujumbe maalumu wa umoja huo upo mjini Ougadougou kwa mazungumzo na serikali ambapo unatarajiwa kutia kiasi cha euro milioni nane kwa serikali mwishoni mwa mwaka huu.

Viongozi hao wamefanya mazungumzo na viongozi wa serikali ya rais Blaise Compaore ambapo wameahidi kufanya marekebisho katika mfumo wake wa mahakama na usalama kwa lengo la kuboresha demokrasia nchini humo.

Mkutano huo baina ya viongozi wa Umoja wa Ulaya na serikali ya Bukinafaso unakuja kufuatia mwezi wa pili mwaka huu serikali ya rais Compaore kushuhudia wanajeshi wakiasi na kusababisha kulivunja baraza lake la mawaziri zaidi ya mara mbili.

Umoja wa ulaya pia umeitaka nchi hiyo kuunda tume mpya ya uchaguzi kufuatia ile iliyopo kulalamikiwa katika uchaguzi wa mwezi wa 11 mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.