Pata taarifa kuu
KENYA-DADAAB

Vurugu zatanda katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya

Wakimbizi wawili wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa nchini Kenya katika kambi ya Dadaab kufuatia kuzuka kwa vurugu baina ya polisi na maelfu ya wakimbizi katika kambi hiyo.

Kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyoko nchini Kenya
Kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyoko nchini Kenya UNHCR
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi katika kambi hiyo Adrian Edward, amesema kuwa vurugu hizo zilizuka kufuatia polisi kuanza kutawanya vikundi vya wakimbizi waliokuwa wakisubiri msaada wa chakula na kutaka kuanza vujo.

Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya maelfu ya wakimbizi ambao walikuwa wamekusanyika katika eneo moja ambalo Shirika la Chakula Duniani lilikuwa likigawa chakula kwa familia ambazo zinaishi katika kambi hiyo.

Msemaji wa polisi katika kambi hiyo amesema kuwa polisi walilazimika kutmia mabomu ya mchozi baada ya kuona wakimbizi hao wakitaka kutumia nguvu kuvamia gari lililokuwa likitumika kugawa chakula ambapo baadae pia waliamua kutumia risasi za moto kwa kupiga hewani kuwatawanya wakimbizi hao.

Kwa mujibu wa shirika la madaktari wasio na mipaka wanaohudumu katika kambi hiyo wamesema kuwa huenda idadi ya wakimbizi katika kambi hiyo ikaongezeka mara mbili ya sasa ambapo kuna wakimbizi zaidi ya laki nne na elfu hamsini.

Ongezeko hilo la wakimbizi nchini humo linatokea wakati ambapo nchi nyingi za ukanda wa afrika mashariki na kati zimekumbwa na ukame huku mgogoro wa kisiasa nchini Somalia ukichangia kuongezeka kwa wakimbizi zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika linaloshughulikia wakimbizi duniani UNHCR imesema kuwa ongezeke la wakimbizi zaidi katika kambi ya Dadaab kunatokana na kujaa kwa kambi zilizoko nchini Ethiopia na kuwa kunahitajika maeneo zaidi ya kuwahifadhi maelfu ya wananchi wanaokimbilia nchini Kenya.

Kambi ya Dadaab ni moja kati ya kambi kubwa zaidi inayohifadhi wakimbizi barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.