Pata taarifa kuu
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC

Mji wa Lubumbashi wazipokea sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya uhuru wa DRC

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaadhimisha alhamisi hii Juni 30, 2011, miaka 51 tsangu ijipatie uhuru wake kutoka kwa mkoloni Mbeleji. Sherehe rasmi mwaka huu zinafanyika katika mji wa pili wa nchi hiyo Lubumbashi badala ya Kinshasa, ni kusini kaskazini mwa nchi hiyo. Rais Joseph Kabila anajielekeza katika mji huo ulioshuhudia machafuko katika usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wakati ghala moja la madini lilipo shambuliwa na “kundi la majambazi” Shambulizi hilo ni la pili kutokea katika kipindi cha miezi 6 baada ya lile lililotokea mwezi Februari kwenye uwanja wa ndege wa mjini hapo ambapo ghala la silaha liliporwa.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, tarehe 30 Juni 2010.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, tarehe 30 Juni 2010. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Gwaride la kijeshi litafanyika alhamisi hii Juni 30, 2011 katika kuadhimisha siku kuu hiyo mjini hapo Lubumbashi, Mji ambao sasa wajipatia umaharufu siku hizi za nyuma na kutajwa kuwa mji mkuu wa nchi hiyo.

Mbali na miji hiyo miji mingine pia iliwahi kupokea sherehe za kitaifa za kuadhimisha siku kuu ya uhuru, ambapo ni fursa pia kwa rais wa jamuhuri kuwahutubia wananchi.

Ujumbe wa rais Kabila kwa raia wake katika kuadhimisha siku kuu hiyo utakuwa ni wa mwisho wa muhula wake huu ambao unamalizika mwezi Novemba ambapo wananchi watapiga kura ya kumchaguwa rais mwingine, Rais Kabila akiwa miongoni mwa wanaowania.

Siku kuu hii ya uhuru wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo inafikia wakati wa mijadala mbalilbali ya kisiasa kuhusu hatma ya nchi hiyo ambapo wananchi wanakodolea macho na masikio kusikiliza kinachonedelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.