Pata taarifa kuu
Senegal-Dakar

Wananchi wenye hasira wateketeza kwa moto ofisi za shirika la umeme mjini Dakar

Wananchi wenye hasira nchini Senegal wamechoma moto majengo ya serikali zikiwemo ofisi za Shirika la Umeme nchini humo wakati wa maandamano yao ya kupinga kukatwa kwa nishati hiyo kwa muda mrefu.

Maandamano mjini Dakar
Maandamano mjini Dakar REUTERS/Finbarr O'Reilly
Matangazo ya kibiashara

Ghasia hizo zimeshuhudia maofisa wanne wa Shirika la Umeme wakijeruhiwa vibaya sambamba na magari manne ya shirika nayo yakichomwa moto jeshi la Polisi nchini humo limethibitisha.

Maandamano ya adhabu ya kukosekana kwa umeme kwa muda mrefu kwenye nchi hiyo yalianzia kwenye Mji wa Mbour uliopo kilometa themanini kutoka Dakar na kisha kusambaa na kuwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi na maji ya upupu kuwasambaratisha.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.