Pata taarifa kuu
Libya, Benghazi

NATO yazidisha mashambulizi mjini Tripoli, mlipuko wa bomu watikisa Benghazi

Mashambulizi mapya ya NATO dhidi ya utawala wa Muamar Gadaffi, yamefanyika mapema leo asubuhi jijini Tripoli, wakati Umoja wa Mataifa ukimshutumu Muamar Gadaffi na waasi kusababisha mauji nchini humo. Mlipuko wa bomu umeutikisa mji wa Benghazi kulioko ngome ya waasi

AFP PHOTO / Imed Lamloum
Matangazo ya kibiashara

Milipuko sita imesikika jijini Tripoli asubuhi hii, ikiwa ni wiki moja sasa ya mfululizo ya mashambulizi ya NATO dhidi ya uwatala wa Muamar Gadaffi, wakati mlipuko mwingine ukitikisa mji wa Benghazi karibu na hoteli moja iliko makao makuu ya waasi.

Msemaji wa serikali ya Gadaffi, Mussa Ibrahim amesema kuwa tangu majeshi ya NATO yaanze kushambulia Libya zaidi ya watu mia saba wanahofiwa kuaga dunia na kuwajeruhi zaidi ya elfu nne.

Wakati huo huo, waziri wa mafuta katika serikali ya Gadaffi Shukri Ghanem amekuwa afisaa mwingine kujiondoa katika serikali ya Gadaffi baada ya kutangaza kujiuzulu kwake akiwa Italia hapo jana na kusema kuwa amefanya hivyo, ili kujiunga na wenzake kupigania demokrasia nchini Libya.

Mashambulizi mapya ya NATO dhidi ya utawala wa Muamar Gadaffi, yamefanyika mapema leo asubuhi jijini Tripoli, wakati Umoja wa Mataifa ukimshutumu Muamar Gadaffi na waasi kusababisha mauji nchini humo.
Wakati Umoja wa Mataifa ukishutmu uongozi wa Gadaffi kutekeleza mauaji, na ukiukaji wa haki za binadamu, huko Benghazi ngome ya waasi wameshtumu majeshi ya Gadaffi kwa mlipuko wa bomu ulitokea hapo jana iliyolenga hoteli moja, shambulizi ambalo halikusabisha mauaji yeyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.