Pata taarifa kuu
Nigeria, Abuja

Watu 10 Wauawa Nchini Nigeria kwa mlipuko wa bomu.

Shambulio la bomu limeripotiwa nchini Nigeria muda mchache kabla ya shughuli za kuapishwa rasmi kwa Rais Googluck Jonathan, kwa muhula mpya wa miaka minne kama rais katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

Shambulio limetokea mjini Abuja
Shambulio limetokea mjini Abuja RFI
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi 10 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya bomu kulipuka karibu na kambi ya jeshi Kaskazini mwa Nigeria.

Maafisa wa uslama wamesema mlipuko huo ulitokea katika soko la Mamy mjini Bauchi siku ya Jumapili. Watu waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.

Mlipuko mwingine ulitokea katika klabu cha pombe viungani mwa mji wa Abuja na kusababisha majeraha madogo, maafisa wanasema.

Hadi sasa haijulikani sababu ya milipuko hiyo, na hakuna kundi lolote ambalo limekwisha jitokeza kudai kuhusika na milipuko hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.