Pata taarifa kuu
SUDAN

Maelfu ya wananchi waendelea kuukimbia mji wa Abyei

Maelfu ya wananchi wa Sudan Kusini wanaoishi katika jimbo la Abyei wameendelea kuukimbia mji huo wakihofia kuendelea kutokea kwa machafuko zaidi.

Baadhi ya eneo la mji wa Abyei likifuka moshi kufuatia mapigano yanayoendelea
Baadhi ya eneo la mji wa Abyei likifuka moshi kufuatia mapigano yanayoendelea Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri anaejihusisha na maswala ya kijamii wa Sudan Kusini James Kok Ruea amesema kuwa mpaka sasa jumla ya wananchi walioukimbia mji huo imefikia watu zaidi ya laki moja na nusu na kuongeza kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka.

Waziri huyo amesema kuwa ongezeko la wananchi hao kuukimbia mji huo kunatokana na kile ambacho wanajeshi wa Sudan Kaskazini wamekuwa wakiwafanyia wananchi wa jimbo hilo ikiwemo vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto.

Juma lililopita mji huo umeshuhudiwa ukiwa katika mapigano baina ya majeshi ya Sudan Kaskazini na Kusini katika kuuwania mji wa Abyei ambao una utajiri mkubwa wa mafuta ambao sehemu zote unadai uko chini yake.

Umoja wa mataifa UN umeviagiza vikosi vya Sudan Kusini kuondoka katika mji huo lakini vikosi hivyo vimeendelea kukaidi agizo hilo huku azimio hilo likisisitizwa  na rais Omary Hassan Al-Bashir.

Vurugu hizo zinakuja wakati ambapo ikiwa umebakia mwezi moja kushuhudia Sudan Kusini ikitangazwa kuwa nchi huru ikijitenga toka Sudan Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.