Pata taarifa kuu
Marekani, Ufaransa, Libya

Marekani na Ufaransa zapania kumaliza kazi nchini Libya huku NATO ikizidisha mashambulizi

Viongozi wa nchi za Marekani na Ufaransa zinasema kuwa zinaungana kuhakisha kuwa wanamaliza kazi, nchini Libya kuhakikisha kuwa kiongozi wa Libya Muamar Gadhaffi, anaondoka mamlakani.Kwa mara nyengine tena, ndege za Jumuiya ya Kujihami ya NATO zimefanya mashambulizi katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. NATO imekuwa ikijaribu kumuondoa madarakani Gaddafi kufuatia uasi dhidi ya kiongozi huyo ulioanza zaidi ya miezi miwili iliyopita. 

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, Uingereza imethibitisha matumizi ya helikopta zake za kijeshi za Apache nchini Libya. Uamuzi huu unaashiria hatua muhimu katika mkakati wa NATO, ambayo hadi sasa imekuwa ikitumia ndege za kijeshi tu katika mashambulizi yake.

Tayari Ufaransa ilishasema kwamba inaunga mkono mashambulizi ya helikopta dhidi ya vikosi vya Gaddafi.

00:33

BARACK OBAMA LIBYA

Rais Barrack Obama wa Marekani, na Nicolas Sarkozy wa Ufaransa wakiwa katika mkutano wa nchi nane tajiri ulimwenguni, G8 huko Ufaransa wamesisistiza kuwa uongozi wa serikali ya Gadhaffi umepitwa na wakati na ni sharti ang'atuke mamlakani, kama anavyoleza rais Obama hapa.

Matamshi hayo pia yameungwa mkono na rais Sarkozy ambaye ameunga swala hilo.

Rais Sarkozy amesema anapanga kuzuru katika ngome ya waasi nchini libya Benghazi, na waziir mKuu wa Uingereza David Cameroon.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.