Pata taarifa kuu
Côte d’Ivoire

Wafuasi zaidi ya 15 wa Laurent Gbagbo waalikwa kwenye sherehe za kuapishwa Ouattara.

Rais wa Côte d’Ivoire Alassane Dramane Ouattara ataapishwa kesho siku ya jumamosi Mjini Yamoussoukro mbele ya waarifiwa kutoka nje na ndani ya nchi hiyo. Mingoni mwa wageni wa ndani wapo wafuasi wa chama cha (FPI) cha Laurent Gbagbo rais wa zamani wa nchi hiyo ikiwa ni moja kati ya juhudi za kutafuta maridhiano ya kitaifa.

Rais Alassane Ouattara, Ijumaa Mei 6, 2011.
Rais Alassane Ouattara, Ijumaa Mei 6, 2011. AFP / Issouf Sanogo
Matangazo ya kibiashara

Sherehe hizo za kuapishwa rais Ouattara zitafanyika chini ya kauli mbiu” Côte d’Ivoire yenye kukusanyika.” Ouattara aliapishwa Mei 6 mjini Abidjan miezi 5 baada ya uchaguzi wa Novemba 28. Muda wote huo kisha kufanyika duru ya kwanza na ya pili ya uchaguzi ulifuatiwa na vurugu zilizo komeshwa baada ya kukamatwa kwa rais Laurent Gbagbo April 11 kwa muda wa siku 10 za mapambano baina ya wanajeshi wa Laurent Gbagbo na vikosi vya FRCI tiifu kwa Ouattara waliosaidiwa na vikosi vya wafaransa vya licorne na vile vya Umoja wa Mataifa vya ONUCI.

Maridhiano

Laurent Gbagbo bado amesalia chini ya kizuizi cha kifungo cha ndani katika Mji wa Korhogo kaskazini mwa nchi hiyo. Zaidi ya wafuasi wake 100 wa chama cha FPI nao pia wanazuiliwa kifungo cha ndani. Lakini hata hivyo kuna baadhi ya wafuasi wa chama hicho ambao wapo huru hawaeshi kwa kujificha. Miongoni mwao ni spika wa bunge Mamadou Koulibaly. Kamati inayo andaa sherehe hiyo imetowa kadi zaidi ya 15 za mualiko kwa wafuasi wa chama cha FPI. Baadhi walipenda kuwepo ili kudhihirisha kabisa nia ya kueleka katika maridhiano ya kudumu licha ya kwamba chama cha FPI cha Laurent Gbagbo hakijakubali rasmi ushindi wa Alassane ouattara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.