Pata taarifa kuu
LIBYA-MAREKANI

Hali ya kibinaadam yazidi kuwa mbaya nchini Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa juhudi za kusitisha mapigano nchini Libya zimeshindikana na hali ya kibinaadam inazidi kuwa mbaya kila kukicha.

Reuters/Tobias Schwarz
Matangazo ya kibiashara

Bwana Ban amesema mjumbe wake maalum nchini Libya Abdul Illah al-Khatib amekuwa akifanya kila awezalo kuushawishi uongozi wa Muamar Ghaddafi kusitisha mapigano bila mafanikio.

Katibu mkuu huyo amesema anahofu na namna mambo yalivyo katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Misrata ambao umekuwa ukishuhudia mapambano makali na mamia ya watu wamepoteza maisha.

Kwa upande wake katibu mkuu wa majeshi ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO Andres Fogh Rasmussen amesema uwezo wa kijeshi wa Ghaddafi umedhoofishwa na hivyo wakati wowote uongozi wake unaweza kuanguka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.