Pata taarifa kuu
LIBYA

Waasi nchini Libya wauteka Uwanja wa Ndege wa Misurata

Waasi nchini Libya wamefanikiwa kuuweka chini ya himaya yao Uwanja wa Ndege wa Misurata baada ya mapigano makali kati yao na Majeshi ya Kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi ikiwa ni mafanikio yao ya kwanza baada ya majuma kadhaa ya kurudishwa nyuma.

Wananchi ambao wamejitolea kwa ajili ya kujiunga na Waasi katika Jiji la Benghazi wakiwa kwenye mazoezi
Wananchi ambao wamejitolea kwa ajili ya kujiunga na Waasi katika Jiji la Benghazi wakiwa kwenye mazoezi
Matangazo ya kibiashara

Uwanja wa Ndege wa Misurata ambao umekuwa chini ya uangalizi wa Vikosi vya Serikali ya Kanali Gaddafi kwa miezi zaidi ya miwili ulikuwa uwanja wa mapambano usiku wa kuamkia leo na hatimaye waasi wakafanikiwa kuteka.

Mashambulizi hayo ya kufanikisha kuuteka Uwanja wa Ndege wa Misurata ambao ni Jiji la tatu kwa ukubwa imeshuhudia wanajeshi watatu wa Kanali Gaddafi wakipoteza maisha.

Msemaji wa Waasi nchini Libya, Abdel Busin amethibitisha kuuteka Uwanja wa Ndege baada ya mapigano makali na wamewarudisha kwa kilometa 15 wanajeshi wa Kanali Gaddafi.

Waasi baada ya kufanikiwa kuuteka kwa mara ya kwanza Uwanja huo wa ndege wameonekana wakishangilia mitaani na kujisifu kwa hatua ya kuvirudisha nyuma Vikosi vya Kanali Gaddafi.

Vikosi vya Kanali Gaddafi navyo havikuwaacha salama Waasi kwani juma ya wanamgambo wao 13 walijeruhiwa vibaya kwenye mapigano hayo ambayo yameshuhudia vifaru kadhaa vikiharibiwa.

Makundi ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Libya yameonya hali ya kibinadamu imezidi kuwa mbaya kutokana na watu 500,000 kuhitaji chakula na matibabu haraka.

Wakati huo huo Majeshi ya kanali Gaddafi yamefanikiwa kuwaua Waasi 2 na kuwajeruhi wengine 15 katika mapigano makali yaliyotokea katika eneo la Zintan.

Tayari Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO yamesema yataendelea na kazi yao ya kuwalinda wananchi licha ya hapo awali kutuhumiwa mashambulizi yao kuwa na nia ya kutaka kumuua Kanali Muammar Gaddafi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.