Pata taarifa kuu
MISRI

Watu 12 wapoteza maisha nchini Misri kwenye mapigano ya kidini

Mapigano ya kidini ambayo yametokea nchini Misri yamesababisha vifo vya watu kumi na mawili huku wengine zaidi ya mia mbili thelathini wakijeruhiwa Kaskazini Magharibi mwa Mji Mkuu Cairo.

Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika Wilaya ya Imbaba iliyopo kwenye Jiji la Cairo baada ya kutokea mapigano ya kidini
Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika Wilaya ya Imbaba iliyopo kwenye Jiji la Cairo baada ya kutokea mapigano ya kidini Reuters/Asmaa Waguih
Matangazo ya kibiashara

Maiti ambazo zimetambuliwa hadi sasa ni nne wa Waumini wa Kikristo, sita za Waumini wa Kiislam huku maiti mbili zikiwa bado hazijatambulika hadi sasa na upepelezi unaendelea.

Waumini wa Kiislam na Kikristo walianza mapigano baada ya kushambuliwa kwa Kanisa la Mtakatifu Mena lililopo katika eneo la Imbaba baada ya uwepo wa taarifa za kuzuiliwa kwa mwanamke ambaye alikuwa anataka kubadili dini kuwa muislam.

Serikali ya Misri imeshatangaza itatumia nguvu zake zote katika kuhakikishan wanakabiliana na machafuko hayo ili amani na utulivu viweze kurejea katika nchi hiyo.

Tayari nchini mbalimbali zimeshaanza kulaani mapigano hayo ambayo yametokea katika sehemu ya kuabudu ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu UAE Anwar Mohammed Gergash ametaka ulinzi na usalama uimarishe.

Vyombo vya habari vya Misri kwa upande wake zimesema kile ambacho kinafanyika ni vitendo vya siri vya wanaopinga mapinduzi kutaka kuleta ghasia katika nchi hiyo.

Naye Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel nchini Misri Mohamed El Baradei amewaita watu hao kuwa ni “Watu wenye Msimamo Mkali katika zama za Kale”.

Kiongozi Mkuu wa Dini ya Kiislam nchini Misri Mufti Ali Gomaa amenukuliwa akionya huenda ikaibuka vita vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa hilo iwapo mapigano haya ya kidini hayatazuiliwa haraka.

Misri imekuwa ikishuhudia mapigano ya kidini mara kwa mara na kuchangia kusababisha vifo na majeraha kwa wananchi wengi wasio na hatia katika nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.