Pata taarifa kuu

Upinzani walaumiwa kuhusika katika vurugu nchini BourkinaFaso

Upinzani walaumiwa na chama tawala nchini Burkina Faso kuhsika katika vurumai ambazo zimekuwa zikishuhudiwas nchini humo.

Maandamano mjini OuagadougouJumamosi April 30, 2011
Maandamano mjini OuagadougouJumamosi April 30, 2011 AFP PHOTO / AHMED OUOBA
Matangazo ya kibiashara

Chama Tawala nchini Burkina Faso anachotoka Rais Blaise Compaore kimeituhumu Kambi ya Upinzani nchini humo kuandaa mpango wa kutaka kufanya mapinduzi ambayo yalishindwa kufanikiwa licha ya uwepo wa maandamano.

Kiongozi wa Chama hicho cha CDP Roch Marc Christian Kabore amesema wamebaini hilo kutokana na kufuatiali nyendo za wale ambao wamepanga na kutekeleza maandamano yaliyoitikisa Burkina Faso.

Kauli hii inakuja baada ya Upinzani siku ya jumamosi kutangaza hatua ya kutaka Rais Compaore aondoke madarakani baada ya kushika wadhifa hao tangu mwaka elfu moja mia kenda na themanini na saba.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.