Pata taarifa kuu
Kampala

Museveni azionya nchi za magharibi

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni azikemea vikali nchi za magharibi kujiingiza katika maswala ya Afrika. 

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. AFP Photo/Marc Hofer
Matangazo ya kibiashara

Shutuma hizo zimekuja baada ya Nchi za magharibi na mashirika ya haki za binadamu kuishutumu vikali serikali ya Uganda na kitengo cha polisi kuhusika na vitendo vya kutumia nguvu hasa risase katika kuwatawanya wanaandamanaji.

Akizungumza na RFI, rais Museveni amesema lazima nchi hizo ziachane na maswala ya Afrika kwa kuwa mambo hayo yako chini ya muungano wa umoja wa Afrika ambao haujashindwa kutatua mizozo.

Serikali ya Uganda inashutumiwa kuhusika na vitendo vya kuwanyima haki ya kuandamana wapinzani na badala yake kuwapiga. Museveni amesema hatovumilia vurugu zinazotokea nchini mwake.

Muungano wa upinzani unaongozwa na Dr kizza Besigye umekuw ukiandamana katika kupinga kile unachosema uhaba wa hali ya maisha na serikali ya Uganda kutowajali wananchi wake kwa kupandisha bei ya bidhaa mahitajio.

Kuhusu mzozo wa libya Rais Yoweri museveni amesema kwamba uingiliaji wa nchi za magharibi katika mzozo huo ndicho kinachosababisha suluhu kutopatikana kwani Umoja wa Afrika ulitoa pendekezo ambalo lilipuuzwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.